Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kanisa Kubwa
Kanisa Kubwa
Kanisa Kubwa
Ebook216 pages3 hours

Kanisa Kubwa

Rating: 4 out of 5 stars

4/5

()

Read preview

About this ebook

Shetani anatka kanisa lako kubakia ndogo. Jinsi una watu wachache katika mkutano wako ndivyo alivyo na mateka wengi. Kima cha kanisa lako kinakuonyesha ni kwa kiwango kipi unapunguza idadi ya watu jehanamu. Wakati una kanisa kubwa, inamaanisha kwamba unajenga roho. Pia inamaanisha kwamba roho zaidi zimeepuka mikono ya shetani. Jua mengi katika hiki "cha lazima" kwa wachungaji wote.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613958551
Kanisa Kubwa
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Kanisa Kubwa

Related ebooks

Reviews for Kanisa Kubwa

Rating: 4 out of 5 stars
4/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kanisa Kubwa - Dag Heward-Mills

    1. 1.Ni lazima utamani kuwa na kanisa kubwa kwa sababu hili ndilo lengo na maono yafaayo zaidi kwa Mchungaji.

    Maono bora na shauku kubwa kwa kila mchungaji ni maono ya kuwa na kanisa kubwa. Kwa nini usiwe na kanisa kubwa kama unaenda kuwa na kanisa?

    Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

    Mithali 29:18

    2. 2.Ni lazima utamani kuwa na kanisa kubwa kwa sababu shauku ya kuwa na kanisa kubwa itakuongoza kwenye safari itakayolifanya kanisa lako likue.

    Kuwa na shauku ya miujiza itakuongoza kwenye matokeo maalumu ya kupata miujiza katika huduma yako. Kuwa na shauku ya kuwa na upako itakuongoza kwenye matokeo maalumu ya kupata upako. Shauku ya ukuaji wa kanisa itakuongoza kwenye safari ya uvumbuzi itakayolifanya kanisa lako likue.

    Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

    Marko 11:24

    [Tafsiri ya Kiingereza husema, "Kwa hiyo nawaambieni, MAMBO YOYOTE MNAYOYATAMANI,wakati mwombapo, aminini kuwa mwayapokea, na mtayapata.]

    Marko 11:24

    3. 3.Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu hatima ya kinabii ya kila kanisa ambalo Bwana hulijenga ni kuwa na mwisho mwema kuliko mwanzo wake.

    Usikatishwe tamaa na udogo wa kanisa lako kwa sasa. Imetabiriwa kuwa mwisho wa huduma yako utakuwa na utukufu mwingi zaidi kuliko mwanzo wake.

    Kwa kuwa neno la Mungu hutabiri kuwa utukufu wa nyumba ya baadaye utakuwa mkubwa kuliko utukufu ule wa mwanzo, ni lazima utarajie jambo lenye utukufu zaidi kuliko lile uliloliona mwanzoni. Mungu atafanya jambo kubwa na atalizidisha kanisa.

    Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini MWISHO WAKO UNGEONGEZEKA SANA.

    Ayubu 8:7

    4.Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu wachungaji wengi wamedanganywa kwa kudhani kuwa kazi imeshafanywa wakati bado haijafanywa.

    Wakati wa kipindi cha huduma yake, Yesu alitoa tamko muhimu sana.

    … Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.

    Mathayo 9:37

    Hii humaanisha kuna roho nyingi za kuvuna. Kuna kazi nyingi kwa ajili yetu sote. Kuna watu wengi wa kujaza makanisa yetu.

    Wachungaji wengi wamedanganyika kwa ukweli kwamba kumbi zao ndogo zimejaa. Watumishi wengi hujisikia kwamba wamekwishakufika kwenye huduma. Unapokea mshahara mzuri na una gari zuri. Mungu amekubariki na unalipiwa mahitaji yako yote. Hii haioneshi kwamba umekwisha kufika. Usimruhusu Ibilisi akupofushe macho yako kwa kazi halisi tunayotakiwa kuifanya. Shetani ndiye anayeshabikia kanisa lilale!! Hunong’ona kwenye mioyo ya watumishi wengi: Kila kitu kiko SAWA. Ndivyo ilivyo. Umefanya. Huu ndio umbali unaoweza kwenda. Hiki ndicho kila kitu unachoweza kufanya kwa ajili ya Mungu! Watumishi wa namna hiyo macho yao ya kiroho na ya kimaono yameshapofushwa na Shetani.Adui huwanong’oneza kwenye mioyo yao, Kila kitu kiko sawa. Ndivyo ilivyo! Umefanya!

    Shetani anataka kanisa lako libaki dogo. Kadri unavyokuwa na watu wachache kwenye kanisa lako, ndivyo anavyokuwa na mateka wengi. Ukubwa wa kanisa lako hukuonesha ni kwa kiasi gani unapunguza sana idadi ya watu Jehanamu. Unapokuwa na kanisa kubwa, ina maana kwamba unaimarisha roho nyingi. Vile vile humaanisha kwamba roho nyingi zimeponyoka kutoka kwenye makucha ya Ibilisi.

    5. 5. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu mapenzi ya Mungu ni kuwa Nyumba yake ipate kujaa.

    Makanisa mengi hayajai kwa sababu siyo makanisa makubwa.

    Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, NYUMBA YANGU IAPTE KUJAA.

    Luka 14:23

    Katika Luka 14, Bwana alitupatia ufunuo muhimu. Bwana alimwambia mtumwa wake, Nahitaji nyumba yangu ipate kujaa. Bwana katika habari hii humwakilisha Yesu. Yesu alihitaji nyumba yake ipate kujaa. Kwa maneno mengine, Yesu hutaka makanisa yake yapate kujaa. Mungu hutaka makanisa yaliyojaa! Bwana katika habari hii hakuridhika kuwa na watu wachache kwenye sherehe yake. Hata hivyo, angeweza kufanya sherehe, lakini alitaka watu wengi zaidi. Na zaidi ya yote, hasa alitaka nyumba ipate kujaa.

    Kwa kupitia hadithi hii, Mungu anaonesha mapenzi yake kwa kanisa. Mapenzi yake ni watu wengi! Mapenzi yake ni vyumba vilivyojaa! Mapenzi yake ni makanisa yaliyofurika! Mapenzi yake ni KANISA KUBWA!

    6. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu shamba lako la mavuno ni dunia.

    Mungu hakututuma twende kwenye vitongoji vya mji wako. Wala hakututuma twende kwenye vijiji vichache. Alitutuma twende ulimwenguni kote. Kama tukiwa na shamba dogo la kuvuna, basi tusitarajie pia kiasi kikubwa cha matunda yaliyovunwa.

    Akawaambia, ENENDENI ULIMWENGUNI MWOTE, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

    Marko 16:15-16

    Ukweli kwamba dunia nzima sharti ifikiwe, humaanisha kwamba mavuno ya roho tutakayoyaleta lazima yawe mengi sana. Kwa yakini yatakuwa ni sehemu kubwa kabisa ya idadi ya watu duniani. Kama sehemu kubwa ya idadi ya watu duniani inapaswa kuokolewa kupitia mahubiri ya injili, basi kila kanisa lazima lijae hata kwenye maungio ya kuta zake kwa kukosa nafasi. Kumbuka ya kwamba kuna zaidi ya roho bilioni sita huko nje zikitusubiri tuzifikie na injili.

    7. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu mfano wa kibiblia wa makanisa ulikuwa na maelfu ya waumini.

    Je, kanisa la kwanza si mfano mzuri tunaopaswa kuufuata? Ikiwa kanisa la kwanza lilikuwa na watu elfu tatu na watu elfu tano, je, idadi hii haipaswi kutumika kama kielekezi? Ni kweli, idadi hii imeandikwa katika Biblia ili tuweze kujua ni kipi tunacholenga.

    Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

    Matendo 2:42-42

    Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.

    Matendo 4:4

    8. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu kuwa na kanisa kubwa humaanisha kuwa roho nyingi zimevutwa kwenye ufalme.

    Kwenye kanisa kubwa kutakuwa na ibada nyingi, mialiko mingi ya madhabahuni na fursa nyingi za kuokolewa kuliko kwenye kanisa dogo. Je, si lengo la kila mhudumu wa injili kuokoa roho kwa ajili ya Bwana? Je, hiyo si baraka ya ziada iliyoongezwa kwamba kanisa kubwa husababisha wokovu wa watu wengi wanaojiunga nalo?

    9. Lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu katika kanisa kubwa wafanyakazi na watendakazi wengi huachiliwa wafanye kazi kwa ajili ya Mungu

    Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke WATENDAKAZI kazi katika mavuno yake.

    Mathayo 9:37-38

    [Tafsiri ya Kiingereza husema, "Mavuno ni mengi sana, lakini watendakazi ni wachache sana. Hivyo mwombeni Bwana asimamiaye mavuno; mwombeni yeye apeleke WATENDA KAZI ZAIDI kwa ajili ya mashamba yake.]

    Mathayo 9:37-38 (NTL)

    Daima kutakuwa na asilimia fulani ya kundi ambayo ni ya watendakazi halisi. Haijalishi kile ufanyacho au usemacho, asilimia fulani ya kanisa haitahusika katika kazi halisi ya huduma. Daima kutakuwa na washangiliaji na watazamaji. Daima kutakuwa na watoa maoni. Watendakazi watakuwa kwenye huduma daima. Kadri unavyokuwa na umati mkubwa wa watu, ndivyo utakavyokuwa na watendakazi wengi watakaotumwa. Na ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi kufadhili.

    10. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu kupitia kanisa kubwa watumishi wengi wa injili, wachungaji na maaskofu wa kudumu huteuliwa na kuachiliwa kwenda kwenye shamba la mavuno.

    Katika kanisa kubwa mara nyingi kuna programu za mafunzo zinazozalisha watumishi. Kanisa lenye washirika elfu kumi kwa hiyo litazalisha wachungaji wengi kuliko kanisa lenye washirika mia moja. Hakika, mchungaji wa kanisa dogo haelekei kupata watu wa kutosha ambao hutaka kuwa watumishi wa injili.

    11. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu katika kanisa kubwa watu wengi huhusishwa katika maombi dhidi ya nguvu za mfalme wa anga.

    12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;…

    Waefeso 6:12-18

    Unapokuwa na kanisa kubwa, maombi mengi yataenda kwa Bwana. Kwa hiyo, watu wengi wataokolewa na kuimarishwa. Wakati Bwana aliponituma kwenda kuanzisha makanisa Ulaya, alinionesha wajibu mkuu mmoja tuliokuwa tukienda kuufanya katika kuujenga tena ufalme wake katika bara hilo. Unaona, Ulaya imekuwa bara la wakana Mungu. Wamemweka Mungu nje ya fahamu zao. Watu wengi wa Ulaya hawaamini kwamba Mungu yupo.

    Miaka iliyopita, Ulaya ilituma wamishenari duniani [kote]. Lakini sasa, wameanguka katika hali ya chini kabisa ya upofu na uovu wa kipepo. Mungu alinionesha kwamba, moja ya majukumu yetu kama kanisa lilikuwa ni kuachilia maombi kuhusiana na hali ya kanisa huko Ulaya.

    Uwepo wetu katika nchi kama Uswisi, Uholanzi na Uingereza, umesababisha maombezi mengi zaidi yaweze kufanyika katika mataifa hayo.

    Kanisa letu huko Geneva lina mikutano ya maombi ya usiku mzima [ya mkesha] kila Ijumaa, huomba kuanzia usiku wa saa sita hadi saa 12 asubuhi. Wanashiriki katika vita vya kiroho katika nchi ambapo Mungu amesahauliwa.Kadri makanisa mengi kama yetu yaendapo kwa mataifa, basi ndivyo maombi zaidi yatakavyofanyika. Hii ni mojawapo ya sababu za msingi kwa nini kanisa kubwa na tawi la kanisa ni muhimu.

    Wakati kanisa ninalolichunga, Lighthouse Cathedral, lilipokua kwa kiwango fulani, tuliweza kufanikiwa kuwa na mikutano ya maombi ya usiku mzima kila siku. Tulikuwa na vikundi vingi vidogovidogo kanisani, kiasi kwamba iliwezekana kuunda zamu ambapo kila kikundi kimojawapo kati ya vikundi hivi kiliweza kuwa na mkutano wa maombi ya usiku mzima kila siku. Hivyo, tulikuwa na kikundi tofauti kilichoomba kila usiku.

    Kadri kanisa linavyokuwa kubwa, ndivyo vikundi vingi vya maombi vinavyoundwa. Maombi zaidi yanawezekana katika kanisa kubwa! Hii ndiyo sababu Ibilisi anataka kanisa libaki kuwa dogo.

    12. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu kanisa kubwa huzaa umati mkubwa wa watu na umati mkubwa huunda matarajio makubwa.

    Basi, watu walipokuwa WAKINGOJA YATAKAYOTOKEA, wote wakiwaza mioyoni mwao habari za Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo;

    Luka 3:15

    Kupitia uzoefu nimetambua kwamba kadri umati unavyokuwa mkubwa, ndivyo matarajio yanavyokuwa makubwa. Wakati unapokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu wa Mungu, huwa kuna hali ya msisimko, matarajio na imani ya kweli. Kwa nini ni hivi? Hii hutokea kwa sababu imani ya kila mtu huinuliwa kwa yale wayaonayo.

    Mwonekano wa umati mkubwa hushawishi imani na husababisha msisimko. Mwunganiko wa imani ya umati wa watu ni mkubwa kuliko imani ya mtu mmoja tu. Jambo hilo husaidia kumiminwa kwa karama ya Mungu kutoka kwa mtumishi.

    Nimehubiri kwenye makundi madogo madogo na kwenye mikusanyiko mikubwa sana. Mazingira ya kiroho ya hali hizi mbili mara nyingi ni tofauti.

    1313. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu katika kanisa kubwa utakuwa na udhihirisho mkubwa wa miujiza kwa sababu ya umati mkubwa na matarajio makubwa.

    Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule.

    Matendo 8:5-8

    Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao na kulithibitisha lile neno kwa ISHARA ZILIZOFUATANA nalo.

    Marko 16:20

    Popote palipo na imani kubwa, unaweza kutarajia uwezo na miujiza zaidi ya uponyaji. Mara kwa mara Yesu alisema, Imani yako imekuponya. Ni imani ambayo huzaa miujiza! Najua baadhi ya watu hawatanielewa katika hili. Sisemi kwamba Mungu hatembei katika makanisa madogo. Mara nyingi nahudumu katika makanisa madogo, na ninamwona Mungu akitembea katika namna ya ajabu. Kwa hakika Mungu hufanya miujiza kwenye makanisa madogo. Yote niyasemayo ni kwamba, kwa ujumla, panapokuwa na watu wengi, kuna imani zaidi, matarajio zaidi, na hivyo, kuna miujiza zaidi. Ninafikiri hata Mkristo wa kawaida kabisa anaweza kuelewa mantiki hii rahisi.

    Kanisa kubwa humaanisha watu zaidi, jambo ambalo humaanisha imani zaidi, jambo ambalo humaanisha uwezo zaidi, jambo ambalo humaanisha miujiza zaidi, jambo ambalo husababisha shuhuda zaidi!

    Je, wewe hutaki utukufu, uwezo na upako zaidi umiminike katika kanisa lako? Ndugu rafiki mchungaji, mwamini Mungu ili uwe na kanisa kubwa. Unapokuwa na kanisa kubwa, baraka nyingi zaidi zitamiminika kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu kwenda kwa watu wake.

    14. Ni lazima uwe na kanisa kubwa kwa sababu uinjilisti zaidi wawezekana kupitia kanisa kubwa.

    Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.

    1 Wathesalonike 1:8

    Mojawapo ya matokeo ya kuwa na kanisa kubwa ni kwamba uinjilisti hufanyika zaidi. Kanisa letu kuu [la Kiaskofu] limegawanyika katika makanisa madogo kumi na tano hivi. Chini ya kila kanisa dogo, kuna huduma kadhaa na chini ya kila huduma kuna shirika kadhaa.

    Ni sera yetu kwamba kila huduma ifanye angalau mkutano mmoja mkubwa wa injili kila mwezi. Kwa kuwa kanisa letu lina huduma nyingi, kuna uwezekano kwamba mikutano hamsini tofauti

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1