Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1
Ebook35 pages25 minutes

Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Johan Boje, afisa wa jeshi la polisi la Eneo la Kati na Magharibi mwa Jutland, anauawa na dereva anayemgonga na kisha kutoroka mbele ya nyumba yake, usiku mmoja wa manane mwezi Machi. Bosi wake, Axel Borg, ni mmojawapo wa watu wa kwanza kuwasili katika eneo la tukio na hapa, anagundua kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kikatili. Mwanawe Johan Boje mwenye umri wa miaka tisa anasema kuwa aliliona gari na dereva, ambaye anadai alikuwa ni afisa wa polisi. Je, huu ni ubunifu unaofanana na ukweli wa mvulana huyo? Wakati kamera ya upelelezi inapothibitisha madai ya mwanawe, Roland Benito, mpelelezi katika Tume Huru ya Malalamishi ya Polisi, anapewa kesi hiyo. Je, mmoja wa marafiki za Johan alikuwa na nia ya kufanya mauaji hayo ya kinyama?
LanguageKiswahili
PublisherSAGA Egmont
Release dateOct 8, 2019
ISBN9788726283624
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1

Read more from Inger Gammelgaard Madsen

Related to Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1

Related ebooks

Related categories

Reviews for Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 1 - Inger Gammelgaard Madsen

    purchaser.

    Hisia ya Hatia Ichomayo

    Sura ya 1

    Alipozima gari, gereji yote ilinyamaa. Sauti pekee iliyosikika ilikuwa ya pumzi yake iliyokuwa ya kasi kuliko kawaida.

    Taa zilikuwa zimemulika meza ya kufanyia kazi alipoingia. Inaonekana kwamba Lukas alikuwa amefanya kazi kwenye nyumba ya ndege tena bila kuondoa uchafu baada ya kukamilisha shughuli zake. Kulikuwa na mavumbi ya mbao kila mahali na msumeno haukuwa umerejeshwa mahali pake kwenye zana zilizokuwa ukutani. Inaonekana kuwa mwanawe alikuwa amekata tamaa na mradi wake - kwa mara nyingine. Alifurahia kidogo akifahamu kwamba angalau alikuwa amejaribu, na sio kukata tamaa tu na kuketi akitazama televisheni au kompyuta. Wavulana wa umri wa miaka tisa wanapaswa kuwa wepesi kufanya shughuli, lakini yeye hakupenda michezo, sio kama Mia ambaye alifanya mazoezi ya mpira wa mikono mara mbili kwa wiki. Bila shaka, alikuwa mkubwa kwa miaka michache, labda hilo lingebadilika wakati ambapo angekuwa mkubwa kidogo.

    Alijipata akiudhika kuwa mwanawe hakuwahi kusikiliza, na kwamba hakuwa amerithi kasi ya vidole ya babake, au tabia yake ya kupenda kuwa na utaratibu. Walikuwa wamechora maumbo ya vifaa vyote kwenye kuta pamoja, hivyo haingekuwa vigumu kupata nafasi ya msumeno. Asidi tumboni mwake ilianza kuchemka na moyo wake ukaanza kupiga kwa kasi zaidi.

    Aliegemea nyuma kwenye kiti chake huku mikono yake ikiwa kwenye usukani, kama aliyekuwa bado anaendesha gari, akafunga macho yake, na kujaribu kuzuia kuudhika kwake  na hasira. Msumemo haukuwa tatizo. Wala purukushani, au Lukas.

    Yeye ndiye aliyekuwa tatizo - kutamauka kwake na maamuzi yake mabaya. Labda kila kitu  wakati huo uliopita hakingetendeka, kama angenyenyekea na kumwambia Alice kila kitu. Alihisi kuwa alikuwa amemshuku kwa muda. Alikuwa ameligundua hilo kila wakati alipochelewa kazini, au alipomwambia kuwa alikuwa ahudhurie mkutano ng’ambo. Alikuwa amejua, lakini hakusema chochote. Je, alimpenda kiasi hicho? Je, alifikiri kuwa hakuwa na watu wengine wazuri zaidi waliomtamani kando na yeye tu? Alikuwa mwanamke mrembo, na angempata yeyote aliyemtaka.

    Alifungua macho yake na kuyakazia kwenye giza. Wivu ulimchoma ndani mwake alipomfikiria Alice akiwa na mwanaume mwingine. Hilo pekee lilimuonyesha jinsi alikuwa mwanaume aliyestahili dharau. Hakuwa na haki ya kuhisi hivyo, wala ya kuhisi faraja iliyomwingia mwilini alipopita jumba hilo la kifahari na kuona kuwa taa zilikuwa zimezimwa, kumaanisha kuwa Alice na

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1