Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4
Ebook36 pages25 minutes

Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Tume Huru ya Malalamishi ya Polisi haijui wapi pa kuanzia. Lakini baada ya kuwahoji bibiye Johan Boje na wenzake, Roland Benito amesadiki kuwa askari huo hakuwa bwana mwaminifu. Huenda muuaji alikuwa na nia zingine kando na zile wanazofuatilia. Wanamhoji mwanawe Johan Boje, Lukas, ambaye alikuwa karibu na mauaji zaidi ya ilivyodhaniwa awali. Upelelezi unachukua mkondo mpya pale ambapo Anne Larsen anapomtafuta Rolando. Anamwambia kile alichogundua, na kuwa anashuku kwamba shauku ya Johan Boje katika moto ule ilikuwa ni ya kibinafsi.
LanguageKiswahili
PublisherSAGA Egmont
Release dateOct 8, 2019
ISBN9788726283594
Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4

Read more from Inger Gammelgaard Madsen

Related to Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4

Related ebooks

Related categories

Reviews for Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hisia ya Hatia Ichomayo - Sura ya 4 - Inger Gammelgaard Madsen

    purchaser.

    Hisia ya Hatia Ichomayo

    Sura ya 4

    Roland Benito alikuwa amewasha taa ya meza yake. Mwangaza uliangaza kwenye karatasi nyeupe na kutoa umbo la miraba minne lenye mwanga mwingi, huku sehemu ya chumba iliyosalia ikiwa na giza.  Kulikuwa usiku sana. Macho yake yaliuma, na alijiambia tena kwa mara yasiyo na idadi kuwa anapaswa kuachana na ripoti na kuelekea nyumani, lakini alikuwa amebakisha ukurasa mmoja pekee.

    Kilikuwa ni kisa cha kusikitisha - Maisha ya familia yakiangamizwa na mlipuko wa gesi. Msichana mwenye umri wa miaka 15 anarudi nyumbani kutoka shuleni na ana muda wa kutosha tu kumuokoa kakake kutoka kwa moto, wakati mamake, Jeanette Løkke, anafariki. Ikiwa Johan Boje kwa hakika alimpenda mwanamke huyu kwa ukweli, kusoma habari hizo lazima kuwe kulimuuma sana. Lakini kwa nini alikuwa anazisoma, ikiwa kesi hiyo ilikuwa imefungwa? Haikuwa na haja. Je, kesi hii ya zamani ndiyo iliyomfanya auawe kikatili? Roland hangeweza kuacha fikira hiyo. Alifahamu kwamba haikuwa lazima atatue mauaji haya. Kazi yake tu ilikuwa ni kujua ni nani aliyekuwa analiendesha lile gari. Hayo ndiyo yalikuwa madhumuni ya uchunguzi huu...hakuna jambo lingine.

    Alikuwa amesisitiza asalie aisome ile ripoti Kaina alipoelekea nyumbani. Alikuwa anataka kubaini ikiwa kulikuwa na dalili yoyote kwamba Johan alikuwa amegundua jambo fulani. Labda kesi hiyo ilikuwa ni mauaji na wala sio mlipuko wa gesi tu. Je, aliyemuua Johan alijua kile alichokuwa amegundua? Labda mfanyakazi mwenzake alimuua? Lakini hakukuwa na taarifa zozote kwenye ripoti - hata kwenye ripoti ya ushahidi pia - ambazo zilidhihirisha hilo. Jeanette Løkke alikuwa amefariki kwenye mlipuko wa gesi, hakukuwa na ushahidi mwingine kando na hilo.

    Roland aliifunga ripoti hiyo na kuegemea nyuma kwenye kiti chake. Alipozima taa ya mezani, alihisi giza ikimzingira hadi macho yake yalipoizoea, na mwangaza wa taa za barabarani ukamfikia.

    Ofisi za Tume Huru ya Kuchunguza Malalamishi ya Polisi zilikuwa kwenye jengo la zamani la Posta na Telegrafu, ambalo lilikuwa sehemu ya kituo kikuu. Kila mtu alikuwa ameelekea nyumbani naye akaamua labda anapaswa kuelekea pia. Kisha atapata muda wa kuzungumza na Irene na labda hata wanye glasi ya Barolo pamoja kabla walale. Hapo kesho, yeye na Karina walikuwa waelekee Silkeborg.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1